IJUMAA KUU : KATIKA MATESO YA BWANA
IJUMAA KUU MASOMO KATIKA MATESO YA BWANA SALA Tuombe haisemwi Ee Bwana, kumbuka rehema zako, na, kwa ulinzi wako wa milele, uwatakatifuze watumishi wako, ambao Kristo Mwanao aliwawekea fumbo la Pasaka kwa kumwaga damu yake. Anayeishi na kutawala milele na milele. AU: Ee Mungu, kwa njia ya mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo, Mwanao, uliangamiza mauti, urithi wa dhambi ya kale, iliyokuwa ikitawala vizazi vyote vya binadamu. Utujalie ili, kwa kufananishwa naye, kama tulivyoichukua sura ya mtu wa udongo kutokana na maumbile, kadhalika tuichukue sura ya mtu wa mbinguni, kwa kutakatifuzwa na neema. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. SEHEMU YA KWANZA: LITURUJIA YA NENO SOMO 1: Isa.52:13-53:12 Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana. Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote, na umbo lake zaidi ya wanadamu), ndivyo atakavyowasitusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo ...